Generali Abdul Fattah al-Sisi akizungumza moja kwa moja kutoka televisheni ya taifa ya Misri
===============
Hatimaye
jeshi la Misri limejitokeza live kwenye televisheni ya Misri na
kutangaza rasmi kuifuta katiba ya nchi hiyo muda mfupi kutoka sasa.
Generali Abdul Fattah Al-Sisi, amesema kuanzia sasa mwanasheria mkuu wa mahakama ya katiba ndiye atakuwa anakaimu madaraka yote ya raisi na kutangaza rasmi kutomtambua bwana Mohamed Morsi.
Wapinzani wa raisi Morsi waliandamana na kukusanyika katika uwanja wa Tahrir Square na kuonekana wakishangilia kwa nguvu wakati Generali Abdul akitoa tangazo hilo la kumpindua raisi Morsi
Mchakato huo wa kumng'oa bwana Morsi ni kufuatia maandamano ya umma ya siku nne kumtaka raisi huyo aachie madaraka na kutii amri ya jeshi ambayo imeisha usiku wa leo jumatano saa nne usiku kwa saa za Tanzania
Aidha kituo cha TV kilichokuwa kikimilikiwa na bwana Morsi cha Muslim Brotherhood kilizimika sekunde chache baada ya Generali Abduli kumaliza hotuba ya kumpindua rais MORSI aliyeingia madarakani baada ya kumpindua aliyekuwa raisi wa nchi hiyo .
No comments:
Post a Comment